Waziri wa Ardhi,nyumba na Maendeleo ya Makazi mh.William Lukuvi ametoa hatimiliki 8,000 za makazi kwa wananchi wa wilaya mbili za Nyamagana na Ilemela mkoani Mwanza,zilizotokana na upimaji wa urasimishaji wa makazi holela katika viwanja 34,940 ambavyo upimaji wake ulianza baada ya agizo lake alilolitoa oktoba mwaka 2016.

Waziri Lukuvi ametoa hati 487 kwa wamiliki wa ardhi eneo la Buhongwa jijini Mwanza,na hati 212 kwa wamiliki wa ardhi eneo la Nyasaka Manispaa ya Ilemela. Ameagiza hati zote zilizotolewa kwenye eneo la Jeshi Nyanshana zifutwe,na manispaa ya Ilemela iwatafutie wahusika viwanja sehemu nyingine ili eneo hilo likabaki kuwa la Jeshi.
Hata hivyo Waziri Lukuvi amempa siku saba mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mary tesha kushughulikia kero za wananchi zilizo ndani ya uwezo wa ofisi yake,huku akimuagiza Kamishna Msaidizi wa ardhi kanda ya ziwa kuorodhesha kero zote ili zishughulikiwe wakati wa ziara yake nyingine,aliyoipa jina la funguka kwa waziri.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: