Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe.Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa Kata ya Nduruma kwenye Mkutano wa hadhara (hawapo pichani) baada ya kuweka jiwe la Msingi kwenye ujenzi wa miundombinu ya Afya katika kituo cha Afya Nduruma.
2
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe.Selemani Jafo(kulia) akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha Dc Ndg.Wilson Mahera Charles pamoja na Mbunge wa Viti Maalum  Mhe. Amina Mollel kwa kusimamia ujenzi wa miundombinu ya Afya kwenye kituo cha Afya Nduruma.
3
Hili ni jengo la wodi ya Kinamama ni mojawapo ya majengo yanayoendelea kujengwa katika uboreshaji wa kituo cha Afya Nduruma.
4
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe.Selemani Jafo(katikati mbele) akisimikwa kuwa Chifu wa Kimaasai maarufu kama Leigwanani wakati wa ziara yake katika kituo cha Afya Nduruma ambapo aliweka jiwe la msingi katika ujenzi wa miundombinu ya Afya.
5
Viongozi wa Halmashauri hiyo wakimskiliza Waziri wa Nchi Mhe.Selamani Jafo akizungumza na wananchi wa kata ya Nduruma.
6
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe.Selemani Jafo akiwaaga  wananchi wa Nduruma baaa ya ziara yake katika Kituo cha Afya Nduruma.
………………
Nteghenjwa Hosseah, Nduruma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Mhe. Selemani Jafo ameagiza ujenzi wa miundombinu ya Afya unaoendelea katika kituo cha Afya Nduruma uongezewe jengo jipya la chumba cha Upasuaji na kile kilichoanza kujengwa kitatumika kwa kazi nyingine.
   
Waziri Jafo amesema hayo wakati alipotembelea kituo hicho na kuweka Jiwe la Msingi katika kituo hicho sambamba na kukagua ujenzi wa majengo mbalimbali ya Afya yanayoendelea kujengwa.
“Nimeridhishwa na ujenzi wa miundombinu hii ya Afya na kazi inaenda vizuri kabisa ila kutokana na hali niliyoiona na mahitaji ya arneo hili naagiza Mjenge jengo jipya la Chumba cha upasuaji na lile ambalo mliliendeleza litatumika kwa matumizi mengine”.
“Baada ya Ujenzi huu kukamilika hiki ndio kituo cha Afya ambacho kitakua kimepata Majengo mengi zaidi katika mpango wetu huu wa uboreshaji lakin yote ni Kwa sababu ya mahitaji ya wananchi wa eneo hili ambao Idadi yao ni kubwa wanaotegemea huduma kutoka katika kituo hiki” Alisema Jafo.
Akizungumza katika Mkutano wa hadhara Mbungu wa viti maalumu anayewakilisha Mkoa wa Arusha Mhe. Amina Mollel amesema Wananchi wa Nduruma wanaishkuru Serikali kwa kuwaboreshea kituo cha Afya Nduruma na wanaomba zaidi msaada wa kupata Gari la kubebea wagonjwa ili iwe rahis kuwatoa katika kituo hicho na kuwapeleka katika Hospital ya Mkoa.
” Mhe Waziri sisi wananchi wa Nduruma tunakushkuru sana kwa namna ambavyo Serikali inatuboreshea huduma za Afya lakini bado shida zetu hazijaisha, tunaomba mtusaidie Gari la kubebea wagonga na matengenezo ya barabara yetu tutashukuru zaidi” Alisema Mhe. Molel.
Waziri Jafo aliahidi kuyashughulia maombi yote yaliyotolewa na Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Mollel na kwa kuanzia amemuagiza Manaja wa Tarura Wilaya kuanza ukarabati mdogo wa barabara hiyo huku wakiendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ukarabati mkubwa na wa kudumu na mahiaji mengine yote ya Afya ameahidi kuyashughulikia kadiri ya upatikanaji wa fedha.
Baada ya ujenzi wa miundombinu hii ya Afya Kituo cha Afya Nduruma kitakua kimepata jengo la Wodi ya Kinamama, Maabara, Chumba cha Upasuaji, Chumba cha kuhifadhia maiti, kichomea Taka, Sehemu ya kufulia na jengo lililokuwa litumike kama chumba cha upasuaji hapo awali litapangiwa matumizi mengine.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: