Washtakiwa 24 kati ya 61 wanaokabiliwa na kesi za ugaidi jijini hapa wamehukumiwa kifungo cha miezi sita jela kwa kosa la kuvua nguo, kisha kugoma kuingia ndani ya chumba cha mahakama kusikiliza kesi zao.

Hukumu hiyo ilitolewa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na hakimu, Nestory Baro ambaye alisema wamehukumiwa kwa mujibu wa kifungu nambari 114 (a) cha mwongozo wa mashtaka ya jinai.

Awali, wakili wa Serikali, Augustino Kombe aliiomba mahakama iwachukulie hatua kali ili iwe fundisho kwa washtakiwa wanaogoma kortini.

Baada ya kauli hiyo, hakimu Baro alisema anatoa kifungo cha miezi sita kwa washtakiwa 24 kati ya 61 ili iwe fundisho kwa wengine watakaoonyesha vitendo hivyo.

Washtakiwa hao 61 wanakabiliwa na kesi ya kujihusisha na vitendo mbalimbali vya kigaidi, kati ya hao 23 kumshambulia nyumbani kwake, Sheikh Sudy Ally Sudi Julai 13, 2014.  
Share To:

msumbanews

Post A Comment: