Baadhi ya wananchi ambao wamejiunga na bima ya afya katika halmashauri ya Busokelo wilayani Rungwe wamelalamikia wauguzi kwenye vituo vya afya vya halmashauri hiyo kuwabagua wagojwa wanaokwenda kutibiwa wakiwa na kadi za bima ya afya na kutoa kipaumbele kwa wagonjwa wanaolipa fedha taslimu hali ambayo wamedai kuwa inakwamisha jitihada za serikali za kuhamasisha wananchi kujiunga na bima za fya nchini.

Wananchi hao wametoa malalamiko yao mbele ya mbunge wa jimbo la Busokelo, Mhe. Atupele Fred Mwakibete kwenye mkutano wa hadhara baada ya mbunge huyo kufika katika kijiji cha Matamba kwa lengo la kukagua ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho.

Akizungumza na wananchi hao, Atupele Mwakibete ameahidi kuyafanyia kazi malalamiko hayo huku akiwahimiza wananchi hao kuungana kukamilisha ujenzi wa jengo la kisasa la zahanati hiyo ambalo kutokana na ubora wake linaweza kubadilishwa na kuwa kituo cha afya.

Katika risala yao wananchi hao wamedai kuwa mbali na ujenzi wa zahanati hiyo pia wanamipango ya ujenzi wa nyumba mbili za wauguzi hivyo wakaiomba serikali pamoja na wadau wengine kuwaunga mkono.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: