Jeshi la polisi wilaya ya Muleba mkoa wa Kagera linawashikilia walimu wa sekiondari wawili kwa tuhuma za kuoa wanafunzi huku mwalimu wa shule ya msingi Kiholele Adrian Musika akikamatwa kwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita katika vichaka baada ya masomo. |
Akithibitisha kuibuka kwa vitendo vya walimu kubaka na kuoa kwa ndoa wanafunzi, Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Luyango amesema kuwa uchunguzi wa ofisi yake umebaini kesi za mimba 24 kati yake sekondari wanafunzi 17 na shule za msingi wanafunzi saba kwa pamoja wameshindwa kuendelea na masomo | |
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba Bw.Emmanuel Shelembi amesema kuwa wadau wa elimu wameadhimia kuboresha elimu kwa kusimamia nidhamu kazini,kudhibiti mimba za utotoni,kujenga maabara,vyumba vya madarasa na nyumba za walimu |
Post A Comment: