USHAHIDI wa video katika kesi inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) jana ulishindwa kuwasilishwa mahakamani baada ya upande wa utetezi kupinga kuwasilishwa kwa sababu shahidi siye aliyeiandaa.


Wakili wa utetezi, John Mallya, akipinga ushahidi wa video wa Ofisa wa Polisi Inspekta Aristides Kasigwa (49), kuwasilishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Arusha, akidai hautakuwa na uhalisia kwa kuwa siye aliyeandaa video hiyo.

Ushahidi uliowekewa pingamizi kuwasilishwa mahakamani hapo ni ripoti ya uchunguzi, mkanda wa video (tape) na CD zinazodaiwa kumrekodi Lema akitoa maneno ya uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli.


Mallya alidai ushahidi huo haustahili kuwasilishwa na shahidi huyo kwa sababu haukidhi matakwa ya kisheria na hauna mahusiano naye.“Huyu sio aliyetuma, wala sio aliyeutengeneza, hivyo ulitakiwa kuwasilishwa na shahidi namba PW 4 ambaye aliutengeneza na kiutuma Dar es Salaam, lakini yeye amekuja hapa mahakamani kutoa ushahidi wake hajawasilisha,” alidai.


Pingamizi hilo liliungwa mkono na wakili mwenzake wa utetezi, Sheck Mfinanga, ambaye aliiambia mahakama  anaunga mkono pingamizi hilo kwa sababu shahidi amekuja mahakamani hapo kutoa ushahidi wa kitu asichokijua na hajui jinsi kilivyotengenezwa.
“Kimsingi hataweza kutuambia juu ya ushahidi huu kwa sababu alitumiwa Dar es Salaam, hajui ulichukuliwaje hataweza kutuambia chochote,” aliongeza. 
Share To:

msumbanews

Post A Comment: