Na Lucas Myovela


Makampuni ya ujenzi 35 yaliyo shida zabuni ya ujenzi wa barabara vijijini leo yamesini mkataba kati yao na wakala wa barabara Tarura mkoa wa Arusha.

Awali mara baada ya kushuhudia zoezizi hilo la kutiliana saini za mikataba hiyo Mkuu wa mkoa  wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo amewaeleza wakandarasi hao walioshinda zabuni hizo kuwa wao kama viongozi ngazi ya mkoa wameweza kutekeleza amri ya mkuu wa Nchi Dk Magufuli ambaye anataka mikataba yote isiwe siri na watanzania wote waweze kujua.


Gambo ameeleza kuwa miaka iliyo pita halmashauri zilikuwa zinalalamikiwa na wananchi kuwa barabara hazina viwango na barabara nyingi kutenhenezwa kisiasa na kuacha za msingi lakini kupitia kwa mkuu wa nchi kuunda Tarura itaenda kutatua changamoto zoto za ujenzi wa barabara vijijini na mijini na taifa kuondokana na uhaba wa barabarazenye viwango vijijini na mijini.


Aidha pia Gambo amewata Wakandarasi hao kuzingatia ujenzi ndani ya muda uliyo pangwa katika mikataba hiyo na kuwataka kufanya kazi kwa uweledi mkubwa na kutoyumbishwa wala kuingiliwa na wanasiasa kwani wao ni tasisi ya kitaalamu na sio taasisi ya kisiasa.


Pia Gambo amebainisha kuwa  ujenzi wa barabara hizo kwa mkoa mzima  wa Arusha ni KM 393.04 kwa halmashauri zote 7 za mkoa wa Arusha kwa viwango tofauti tofauti vya ujenzi wa barabara hizo na gharama zake zote ni Shilingi Bilioni sitana milion aribaini na nne.



Kwa upande wake mratibu mkuu wa Tarura mkoa wa Arusha Mhandisi  Edward Amboka ameeleza kuwa mikataba hiyo kipindi cha nyuma ilikuwa haisainiwi hadharani na palikuwa na changamoto kubwa ya usainishaji ikiwemo rushwa lakini kwa awamu hii ya 5 ya rais Magufuli kuunda tarura mikataba yote itasainiwa wazi.


Pia Mhandisi Amboka aliwataka Makandarasi hao walio shinda zabuni kufanya kazi kwa uweledi wa taaluma yao na kutumia utaalamu wa juu katika kazi zao. "waliyo omba tenda hizo za ujenzi walikuwa 256 lakini nyie kampuni 35  ndio mmeshinda msije mkavuruga kazi za maendeleo ya taifa letu", alisema mhandisi Amboka.


Na kwa niaba ya  wakandarasi hao waliyo shinda tenda hizo Eng Martin Waliyoba ambae ni mkurugenzi mwendeshaji wa  kampuni ya K W Construction Campany Ltd ilipo jiji dar-es-salaam ameishukuru serikali kwa kuweka wazi usainishaji wa mikataba kitu ambacho ni kizuri.

"Niishukuru serikali kwa haya yote kuanzia utangazaji wa tenda hadi leo kunapo ingia katika mikataba ila nadhani ni kazi kwetu sisi kufanya kazi kwa ustawi mkubwa kwaajili ya maendeleo ya taifa letu na pia itatujengea heshima kutokana na ubora wa kazi yako". alisema Eng waliyoba.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: