Jose Mourinho na Antonio Conte kwa muda sasa wamekuwa wakitupiana maneno ya chinichini katika mikutano na waandishi wa habari japo chanzo haswa cha wawili hao kurushiana vijembe hakifahamiki.
Wiki iliyopita kocha wa Chelsea Antonio Conte alimjibu Jose Mourinho ambaye aliongelea tabia ya Conte kuwa na mambo mengi akiwa benchi na Conte akasema hizo huwa ni tabia za Mourinho labda kama anajisema.
Mourinho hakurudi nyuma na jana baada ya ushindi wao wa mabao mawili zidi ya Derby Country aliibuka tena na kijembe kizito zaidi kwa Antonio Conte na safari hii akikumbushia mambo ya upangaji matokeo.
Msimu wa mwaka 2012/2013 Antonio Conte alikumbwa na adhabu ya kufungiwa miezi minne katika soka kutokana na kuhusishwa na upangaji matokeo lakini baadaye mahakama ilimsafisha.
Sasa Jose Mourinho amesema anaweza kufanya mambo yote akiwa benchi na kweli akaonesha tabia mbaya lakini hawezi kufanya kosa la kupanga matokeo hata siku moja, jibu ambalo moja kwa moja linamuendea Antonio Conte.
Tangu Conte ajiunge na Chelsea kuchukua mikoba ya Jose Mourinho kumekuwa hakukaliki kati ya watu hao wawili japo wakikutana huwa wanasalimiana lakini mara zote wamekuwa wakitupiana vijembee.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: