Uongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Njombe wakiongozwa na Katibu wa UVCCM Mkoa Ndugu Sure Mwasanguti umelaani vikali tukio la Katibu UVCCM Wilaya ya Iringa Ngugu Alphonce Muyinga kuchomewa nyumba yake moto na watu wasiojulikana huku tukio hilo likihusishwa na mambo ya Kisiasa.

 Ndugu Mwasanguti katika mahojiano yake na wanaHabari ameutanabaisha Umma kuwa ndani ya siku mbili hizi Mkoani Iringa matukio ya uvunjifu wa Amani yamerindima, kwani kabla ya nyumba hiyo kuchomwa moto ,Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwangata kwa tiketi ya CHADEMA Ndugu Lijuja na sasa kahamia CCM aliharibiwa nyumba yake na watu wasiojulikana. 

Kwa matukio haya mawili yaliyoambatana ni ishara mbaya sana katika siasa za nchi yetu. Katibu Mwasanguti amevitaka vyombo vya dola kulishughulikia suala hili ili kuwabaini wavunjifu wa Amani hao na hatua kali zichukuliwe dhidi yao.

Aidha, Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa kutokea Mkoa wa Njombe Ndugu Omega Thobias licha ya kutuma salamu za Pole kwa Uongozi wa UVCCM Iringa unaoongozwa na Mwenyekiti wake Ndugu Kenani Kihongosi amewaondoa hofu wana Iringa na waTanzania kwa ujumla kwamba matukio haya yasiwarudishe nyuma kwa kuogopa kusonga mbele ila kwa kudra za Mwenyezi Mungu tutakuwa salama na harakati ziendelee kama kawaida huku akiwakaribisha wote wanaotaka kuhama vyama vyao na kuhamia CCM kwani ndio uhuru wenyewe.

 Alisema, "Hii ni Liberty, the freedom to live as you wish", na watu wajue Siasa ni maisha na sio Uadui, Mwishowe akamalizia kwa kusema #TUKUTANE KAZINI.
Katibu wa UVCCM Mkoa wa Njombe alianbatana pia na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Njombe Mjini Ndugu Bi. Devotha Steven na Katibu wa UVCCM Wilaya ya Njombe Mjini Ndugu Daniel
Share To:

msumbanews

Post A Comment: