Mwenyekiti wa kamati ya waamuzi Salum Hamis Umande “Chama” hatimaye amewajibu Azam Madai yao ya kutokuwa na imani na Mwamuzi Israel Mjuni Nkongo mwamuzi ambaye ambaye amepangwa kuchezesha mchezo kati ya Azam Na Yanga siku ya Jumamosi January 27 2018 katika uwanja wa Azam(Azam Complex).

Chama msomaji wa Msumbanews.co.tz amesema hawatambadilisha mwamuzi huyo kutokana na kutoona tatizo lolote kwani ni mwamuzi mwenye anayekidhi vigezo vyote.

” Uwezekano wa kumbadilisha haupo kwani ukiendekeza kubadili waamuzi kila klabu itakuwa inakataa waamuzimwisho wa siku tutakosa waamuzi, Kikubwa mchezo wa Mpira wa Miguu unachezwa hadharani na Kila Mtu anaona kama akiharibu uzuri kamati ipo itamchukulia hatua”

Kuhusu kulaumiwa kwenye mchezo kati ya Mbeya City na Prisons Darby ya Mbeya Hii ambapo mwamuzi huyo alionekana kuboronga kiasi cha kutaka kupigwa na washabiki wa Mbeya City walioamini kuwa ameipendelea Tanzania Prisons Chama amefunguka na Kumtetea kwa kusema Kuwa.

”Huwezi Kumhukumu kwa mechi moja, mpaka sasa kashachezesha mechi karibu tisa za Ligi msimu huu, Mwamuzi ni mwanadamu anaweza akaamka vibaya siku hiyo akateleza kwahiyo tumhukumu kwa michezo mingi alaiyochezesha “

Chama ametoa angalizo kwa vilabu kuwa viache kuwa vinaenda uwanjani vikiwa na matokeo yake mkononi bali viende vikacheze mpira tu uwanjani.

Nkongo amewahi kuchezea kichapo kwenye mchezo kati ya Yanga na Azam uliofanyika March 10 mwaka 2012 mara baada baada ya kufanya maamuzi ambayo wachezaji wa Yanga hawakukubaliana nayo mechi iliyoisha kwa Yanga kufungwa huku wachezaji wake wawili wakipewa kadi nyekundu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: