Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dr. Timoth Wonanje akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Semina hiyo kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa .

Baadhi ya Washiriki wa Semina ya Waganga Wakuu wa Mikoa na Wataalamu wa Radiolojia juu ya Usimamizi wa Matumizi salama ya Mionzi katika Uchunguzi na Matibabu ,semina iliyoandaliwa na Tume ya Mionzi Tanzania na kufanyika jijini Arusha.
Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania  Firimini Banzi akisisitiza jambo katika semina hiyo.
Washiriki wa semina wakiwa katika picha ya pamoja.Picha na Frednand Shayo



Baadhi ya watumiaji wa masuala ya mionzi hawazingatii matakwa ya sheria na kanuni za matumizi sahihi ya mionzi kwa wananchi hali inayoweza kuleta athari kwao pamoja na wanaotoa huduma hiyo ya mionzi. Aidha vifaa vinavyotumia kwaajili ya X, Ray zinapaswa kukaguliwa kila mwaka ili kudhibiti matumizi yasiyo sahihi ya mionzi kwa binadamu na watoa huduma.

Akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Waganga Wakuu wa Mikoa na Mafundi Sanifu wa Mionzi (Radiolojia)  juu ya usimamizi wa matumizi salama ya mionzi katika uchunguzi wa matibabu, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dk,Timoth Wonanje amesema matumizi ya mionzi katika uchunguzi na matibabu yanaleta faida katika afya za umma.

Amesema baadhi ya watumiaji wa mionzi hawazingatii matakwa ya kisheria hali inayoweza kuleta madhara kwa watumiaji,kutokana na ukiukwaji wa sheria za nchi Amesema waganga wakuu wanawajibu wa kuhakikisha wanasimia huduma bora za utoaji wa mionzi ili kudhibiti matumizi sahihi ya mionzi kwa wananchi, watoa huduma hizo kwenye hospitali mbalimbali nchini.

Pia amesisitiza kuwa makadirio ya matumizi ya mionzi duniani yanaweza kuweka idadi ya kila mwaka ya uchunguzi kupitia taratibu za radiolojia kuzidi zaidi ya milioni 3 ya matibabu ya tiba kuzidi zaidi ya milioni 5.

"Mionzi inaweza kusababisha madhara makubwa hivyo mbinu na taratibu zinazozingatia viwango vya Kitaifa na Kimataifa lazima ifuatwe ili kupunguza hatari ya madhara ya mionzi kwa wagonjwa, wafanyakazi, umma na mazingira "


Naye Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania  ( TAEC), Firmin Banzi alisema semina hiyo ya siku mbili wanaotoa kwa waganga wakuu wanawajibu hospitali za mikoa na wataalam wa mionzi kwa kuzingatia sheria ya Nguvu za Atomiki namba 7 ya mwaka 2003 "Amesisitiza changamoto za ubora wa utoaji wa huduma za mionzi ni lazima zitatuliwe ili kudhibiti matumizi sahihi ya nyuklia"     

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dk,Leonard Subi alisisitiza kuwa ni vyema vifaa vya udhibiti wa mionzi ukawepo ili kupunguza madhara kwa watoa huduma sanjari na wananchi.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: