Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika la utangazaji TBC, Tido Mhando, ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Azam Media akiwa katika ukumbi wa wazi  wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akisubiri kusomewa mashtaka yanayomkabili.
 Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika la utangazaji TBC, Tido Mhando, ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Azam Media aksindikizwa kutoka katika ukumbi wa wazi  wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kusomewa mashtaka yanayomkabili. Mhando amekana mashtaka hayo na yuko nje baada ya kutimiza masharti ya dhamana, ambapo Hakimu Nongwa alimtaka mshtakiwa huyo kutoa fedha taslimu mahakamani hapo Sh 444 milioni ama hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.



Aliyekuwa kuwa mkurugenzi Mkuu Wa shirika la utangazaji nchini (TBC), Tido Muhando, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtka ya uhujumu uchumi.
Mhando ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Azam Media anakabiliwa na mashtaka manne ya matumizi mabaya ya madaraka na shtaka moja la kuisababishia serikali hasara  ya zaidi ya sh. Milioni 887.

Mhando alifikishwa mahakamani hapo nyakati za asubuhi na ilipofika saa 5:22 asubuhi aliingizwa katika ukumbi wa mahakama ya wazi kusomewa kesi yake hiyo.  Mhando amesomewa mashtaka yake  na Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai aliyekuwa akisaidiana na wakili, Aneth Mavika pamoja na Dismas Mganyizi.

Akisoma hati ya mashtaka Swai amedai, Juni 16, 2008 huko Dubai, United Arab Emirates (UAE) mshtakiwa Mhando, akiwa mwajiriwa wa TBC kama Mkurugenzi Mkuu alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa makubaliano kwa ajili ya kuendesha vipindi vya utangazaji kati ya TBC na Channel 2 group Corporation ( BV1) bila ya kupitisha zabuni kinyume  na sheria ya manunuzi na kuisabishia  BV1 kupata manufaa.

Katika shtaka la pili imedaiwa, Juni 20,2008  katika eneo hilo,  Mhando, katika utekelezaji wa kazi yake alitumia madaraka vibaya kwa kusaini makubaliano ya utangazaji wa  digital duniani kati ya TBC na BV1

Pia imedaiwa Agosti 11,2008  na Septemba 2008 katika maeneo hayo, Mhando alisaini mkataba wa makubaliano ( kuongea na wakuu wa mkataba ) kwa ununuzi, usambazaji na kufunga vifaa vya usambazi na mnara wa utangazaji kati ya TBC na BVI na kuisababishia BVI kupata faida.

Katika shtaka la nne, Mhando anadaiwa,  Novemba 16, 2008 akiwa Dubai, United Arab Emirates alitumia vibaya madaraka yake kwa kusini mkataba wa makubaliano (kuongea wakuu wa mkataba ) kwa kuendesha miundombinu ya utangazaji ( DTT broadcast infrastructure) kati ya TBC na BVI na kusababisha BVI kupata manufaa.

Katika shtaka la tano Tido anadaiwa kuwa kati ya Juni 16 na Novemba 16,2008 katika maeneo hayo ya United Arab Emirates aliisababishia hasara TBC ya Sh 887, 122,219.19. 

Hata hivyo, mshtakiwa Mhando amekana mashtaka hayo na yuko nje baada ya kutimiza masharti ya dhamana, ambapo Hakimu Nongwa alimtaka mshtakiwa huyo kutoa fedha taslimu mahakamani hapo Sh 444 milioni ama hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.

Aidha ametakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao watasaini bondi ya milioni 500, na pia hatakiwi kutoka nje ya nchi bila ya kuwa na kibali cha mahakama. Kesi hiyo, imeahirishwa hadi Februari 23, 2018 kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali (PH). Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo umekamilika
Share To:

msumbanews

Post A Comment: