Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya Genk ya nchini Ubelgiji amezidi kufanya vizuri uwanjani na hata nje ya uwanja. Wengi watakumbuka kuwa, siku chache zilizopita, Mbwana Samatta alitangazwa kuwa kijana mwenye ushawishi mkubwa zaidi nchini Tanzania.
Kwa upande wa soko la kimpira, Samatta amezidi kuthihirisha ubora wake ambapo sasa kwa mujibu wa mtandao wa transfermarkt.com, thamani ya mshambuliaji huyo ni ni Euro 3 milioni sawa na TZS 8.4 bilioni.
Thamani hiyo ya Samatta ni kubwa kuliko thamani ya vilabu vitatu vya Tanzania, Simba, Yanga na Azam ikiwekwa pamoja. Kwa mujibu wamtandao huo, thamani ya vilabu hiyo kwa pamoja ni TZS 5.1 bilioni (ikijumuisha gharama za usajili).
Kwa mujibu wa mtandao huo, thamani ya Simon Hapyygod Msuva anayechezea klabu ya Difaa El Jadida ya Morocco ni Euro 475,000 (Sh1.3 Bilioni) wakati thamani ya Abdi Banda anayechezea Baroka ya Afrika Kusini ni Euro 300,000 (Sh838 Milioni) wakati Emmanuel Okwi anayekipiga Simba ni Euro 100,000 sawa na TZS 279.8 milioni.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: