Wakili Franciscar Gasper akitoa mada juu ya sheria ya ardhi pamoja na mirathi.
Wanafunzi washiriki semina hiyo kutoka shule za sekondari mbalimbali wilaya ya Halmashauri ya meru
Afisa sheria wa TAWLA Siael Leng'ida akifuatilia mada mbalimbali zilizikuwa zikitolewa ktk semina hiyo.
Pichani ni washiriki wa semina hiyo wakiwa pamoja na wanasheria kutoka TAWLA, ( picha na Lucas Myovela).
Awali akifungua semina hiyo iliyo wahusisha wanafunzi pamoja na walimu wa sekondari katika shule za wilaya ya Meru Afisa sheria wa TAWLA Bi Siael Leng'ida ameeleza kuwa chama cha wanawake wanasheria kinatambua umuhimu wa mwanamke katika jamii na mwanamke anatakiwa kupata haki zote katika jamii kama wanavyo pewa wanaume.
Bi Siel ameonheza kuwa elimu hiyo imefatia baada ya TAWLA kupata mradi uliyoilenga wilaya ya Meru ambapo kwa hivi sasa wilaya hiyo inachangamoto katika sheria za mirathi ya ardhi na jamii kubwa ya meru haimthamini mwanamke katika kumiliki ardhi na kuonheza kuwa kufuatia kwa semina hiyo wameweza kuunda Club za haki ardhi mashuleni wilayani humo lengo likiwa ni kutoa elimu na sheria za ardhi kuanzia ngazi ya chini ili jamii kuweza kutambua uthami wa ardhi na matumizi yake.
"Tunategemea semina hii itakapo isha wanafunzi hawa watakuwa mabarozi wazuri katika jamii hasa kutoa elimu ya sheria ya ardhi na matumizi yake na itawasaidia wenyewe kuitumia vyema ardhi katika kukuza kipato na taifa kunufaika kwa ujumla kwani watakuwa wamewza kutambua uthamani wa ardhi" alisema Siel Leng'ida.
Nae kwa upande wake mtoa mada ambae pia ni mwanasheria wa kujitegemea Bi Franciscar Gasper ameeleza kuwa somo la sheria ya ardhi linapaswa kufundishwa kuanzia ngazi za chini ili mwanafunzia anapokuwa akue katika utambuzi yakinifu wa shiria ya ardhi na itaidia taifa kupiga hatua kubwa.
Aidha Bi Franciscar ameongeza kuwa ili kupunguza migogoro ya ardhi elimu serekali inapaswa kuongeza masomo ya sheria za ardhi kwa kina kuanzia shule za msingi na katika jamii ili kuondoa dhana ya mwanamke hapaswi kumiliki ardhi itasaidia wanafunzi wanapo maliza sekondari kwenda kujiajiri katika kilimo kupitia ardhi za jamii zao zinazo wazunguka.
" Mwanafunzi anapokuwa akisoma huku akijua sheria ya ardhi na mirathi pamoja na thamani yake ni rahisi sana taifa kupiga hatua kwa kasi katika kukuza kilomo na kuzalisha mazao mengi na tanzania kuzalisha ajira kwa vijana kuondoa vizazi tegemezi na Tanzania ya viwanda itaonekana kwa muonekano mpya wa viwanda vya wapiga kazi na kuwa na bidhaa nyingi hapa nchini" alisema Bi Franciscar.
Nao kwa upande wao wanafunzi ambo ni walengwa wa semina hiyo ya sheria ya ardhi wameeleza kuwa elimu waliyo ipata kupita TAWLA hawajawahi kuipata popote pale na wameweza kutambua thamani ya ardhi na kuzitambua sheria za mirathi ya ardhi zinazoeleza haki ya mwanamke katika kumiliki ardhi katika jamii.
Ireen Isanja ni mmoja wa wanafunzi wa kidato cha nne kutoka katika shule ya sekondari ya Ngwalisambu wilayani Meru, yeye anaeleza kuwa upatikanaji wa ardhi kwa wanawake ni mdogo katika jamii lakini kupitia semina hii yeye anao uwezo wa kuimiliki arsdhi katika jamii na kuiendeleza pasipo kujali mila na desturi ninazo tumika kumganadamiza mwanamke kwa kueleza kuwa kumiliki ardhi ni haki kwa kila mmoja pasipo kujali jinsi ya mtu.
Walimu pia hawakuwa mbali katika kuchangia dhidi ya elimu hiyo kutoka TAWLA ambapo nao wameiweza kuomba TAWLA elimu hiyo kwa vijana wanafunzi isiishie hapo na badala yake iendelee hadi vyuoni ili kusaidia mwanamke kupata haki sawa na mwanaume ya kumiliki ardhi na kueleza kuwa wao kama walimu wataendelea kulea clubu za sheria ya ardhi huko mashuleni ipasavyo ili kutoa mchango wao kwa wanafunzi kutojitenga na utegemezi wa ardhi.
TAWLA wamefanikisha hilo katika utoaji wa elimu ya kumiliki ardhi kwa wanafunzi wa shule zaidi ya saba za Halmashauri ya wilaya ya Meru na kuweza kuonyesha njia ya kutetea haki ya.mwanamke katika jamii dhidi ya kumiliki ardhi na kuiendeleza je upi msimamo wa serikali katika jamii ili kuliendeleza hili lililo anzishwa na TAWLA
? Aidha pia semina hiyo ya siku mbili inategemewa kufungwa hapo kesho na wanafunzi hao kuwa mabarozi wazuri katika sheria za ardhi.
Post A Comment: