Home
MICHEZO
Tanzia : Kocha msaidizi wa Mwadui Fc afariki dunia
Kocha Msaidizi wa Mwadui FC, Jumanne Ntambi amefariki dunia mjini Shinyanga.
Ntambi ambaye ni mchezaji wa zamani wa Biashara Shinyanga, amefariki katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga.
Taarifa zinasema aliugua muda mfupi na alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo ambao aliugundua katia hatua a mwisho kabisa.
Hadi mauti yanamkuta jana saa tatu usiku, marehemu alikuwa mwajiriwa wa klabu ya Mwadui FC ambayo uongozi wake umethibitisha kuhusiana na msiba huo.
Back To Top
Post A Comment: