Mtandao wa WhatsApp unazidi kushika kasi katika matumizi mbalimbali kuanzia katika nyanja ya kijamii, kiuchumi na hata kisiasa. Watu hutumiana jumbe mbalimbali zikiwemo za picha, video na maandishi kwa ajili ya kufanikisha lengo la mawasiliano.
Mbali na kutumiana jumbe kati ya mtu na mtu, kuna mawasiliano pia ambayo hufanyika katika makundi ya WhatsApp. Makundi haya yameundwa kwa malengo mbalimbali ambapo kuna mengine yana lengo maalum na kwamba huwezi ukaweka mada myingine tofauti, wakati kuna yale ambayo ni huru mnaweza kujadiliana jambo lolote.
Makundi hayo huwa na viongozi mbalimbali ambao wengi ni wale waliyoyaunda, lakini mara nyingine huwa sio lazima. Viongozi hawa lengo lao kuu ni kusimamia shughuli na mazungumzo kwenye kundi.
Watu wanaopewa dhamana ya kuongoza makundi haya wana tabia mbalimbali. Utofauti wa tabia hizi hufanya kuwapo kwa namna mbalimbali za uongozi. Hapa chini bi baadhi za aina ya viongozi wa makundi ya WhatsApp.
1: Madikteta
Hawa ni wazimamizi wa makundi ya WhatsApp wenye njaa ya kuwa na mamlaka. Hakuna mtu aliyewachagua lakini kila mtu anawaogopa. viongozi hawa wanaendesha kundi kama chombo chao binafsi na jaribio lolote la kuwasilisha maono ambayo hayaungi mkono tabia yao hukabiliwa vikali.
Hawataki kumuacha mtu yeyote kuondoka katika kundi hilo na ukijaribu kuondoka unarejeshwa mara moja. Huwafanya wajumbe katika kundi kujiona kama wapo kifungoni.
2: Mafia
Hawa sio wasimamizi wa kweli, lakini ndio walio na nguvu nyuma ya msimamizi. Wanavunja uhusiano katika kundi hilo na wanaamua ni nani anayefaa kusalia na ni nani hafai.
Wakati maslahi yao yanapokuwa hatarini wanajitokeza na kuchukua uongozi huku wakionyesha muongozo wa kundi husika na wajumbe wengine wanatakiwa kufuata.
3: Waasi
Hawa ni wasimamizi wa makundi ya WhatsApp ambao husahau wao ndio viongozi. Wao ndio wa kwanza kuchapisha picha za fedheha , kuzua uhasama miongoni mwa wanachama walionyamaza na kuwa suluhu.
Kiongozi wa kundi ndiye anayetakiwa kuhakikisha utulivu na muelewano kwa wajumbe wake, lakini viongozi waasi wao ndio wanakuwa wakwanza kitubua mambo.
4: Wanaopenda kufurahisha watu
Hawa ni kinyume na wasimamizi madikteta, wanaukumbatia ulimwengu. Kiongozi anakuwa na msimamo wa wastani, ikimaanisha kwamba kundi hilo huwa na kelele, hakuna msimamizi na sheria hazifuatwi.
Matokeo yake ni kwamba mamlaka yao huchukuliwa na watu wengi wanaotaka kusimamia kundi hilo.
5: Wakosoaji
Hawa ni kama walimu, hufurahia kukosoa namna wajumbe katika kundi wanavyokosea kuandika. Hufanya hivyo mithili ya mwalimu anayewashika masikio wanaofanya makosa kama hayo na kuwarudisha shule.
Bahati yako ni mbaya iwapo huwezi kusahihisha maandishi katika simu yako aina ya smartphone.
Ni wapelelezi wa maswala ya maadili na ujumbe wowote unaotishia watu wazima hutolewa kwa haraka.
Post A Comment: