Rais Donald Trump alichukizwa na maswali ya mwandishi wa kituo cha televisheni cha CNN, Jim Acosta aliyeuliza mara kwa mara kuhusu kauli yake ya kuita mataifa ya Afrika kuwa ni machafu.
Mwishoni mwa hafla ya pamoja na Rais Nursultan Nazarbayev wa Kazakhstan, Trump aliulizwa na Acosta kama alisema katika mkutano wa chama chake kuwa anapendelea zaidi wageni kutoka Norway.
"Nawataka waje kutoka kila sehemu. ...Asante sana," Trump said, wakati maofisa wa Ikulu ya Marekani wakiwataka waandishi kutoka nje.
Baadaye Acosta akamuuliza Trump kama anapendelea wahamiaji kutoka nchi za watu weupe au wa jamii ya kihindi.
"Nje," alijibu Trump, akionyesha kidole sehemu ya kutokea wakati mkutano huo na waandishi ukiisha.
Trump na Acosta walipambana tena mwaka mmoja uliopita baada ya kuchapishwa kwa nyaraka kuhusu uhusiano wa Trump na Russia, huku Trump akisema "nyinyi ni habari za kubuni."
Share To:

msumbanews

Post A Comment: