Stand United imeichapa Mbao FC kwa bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Stand United ilipata bao lake pekee lililofungwa kwa mkwaju wa penalti na Vitalis Mayanga katika dakika ya 40, baada ya Kipa wa Mbao, Ivan Rugumandiye kumuangusha Bigilimana Babikakuhe katika eneo la hatari.
Kwa matokeo hayo, Stand wanafikisha pointi 13 huku Mbao wakibaki na alama zao 15 baada ya mechi 14.

Mbao katika mchezo huo watajilaumu wenyewe kutokana na kucheza kwa mbinu ya kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza, kuliwapa nafasi wapinzani wao kuchochea mashambulizi mfulululizo.

Mchezaji Babikakuhe wa Stand alionekana kuwa mwiba mkali kwa ngome ya Mbao.
Katika mchezo mwingine; Mtibwa Sugar imelazimishwa suluhu na Njombe Mji.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: