Klabu ya soka ya Singida United kupitia kwa Mkurugenzi wake Festo Sanga, wamesema wanajipanga kulipiza kisasi dhidi ya timu ya Mwadui FC ya Shinyanga.

Sanga amesema baada ya mchezo wa jana ambao ulikuwa wa mwisho kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi kuu soka Tanzania Bara, nguvu zao zote wanazielekeza kwenye mechi ya kwanza ya mzunguko wa pili ambapo watakuwa nyumbani dhidi ya Mwadui FC.

''Baada ya kupata ushindi dhidi ya Tanzania Prisons, sasa tunakuja Dar es salaam kucheza na Green Worriors na baada ya hapo macho yetu yote yapo kwenye mchezo wetu wa kulipa kisasi dhidi ya Mwadui FC ambayo ilitufunga mabao 2-1 kwenye mechi ya kwanza'', amesema.

Katika mchezo wake wa kwanza wa ligi baada ya kupanda daraja msimu huu, Singida United ilianzia ugenini kucheza na Mwadui FC ambapo ilikubali kichapo cha mbaao 2-1. Wikiendi ijayo timu hizo zitaanza mzunguko wa pili na mechi yao itapigwa kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida.

Kwa upande mwingine Singida United leo imeanza safari kuja jijini Dar es salaam kwaajili ya mchezo wake wa raundi ya tatu ya kombe la shirikisho ambapo itakutana na wababe wa Simba Green Worriors.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: