Baada ya ushindi wa goli 4-0 dhidi ya Singida United hapo jana Simba kutua Bukoba kwa ajili mchezo wa ligi kuu.

Klabu ya Simba asubuhi ya leo inaratajiwa kusafiri kwa ndege hadi Bukoba kwa ajili ya mchezo ujao wa ligi kuu Tanzania Bara.

Simba inayoongoza ligi kuu kwa jumla ya pointi 29 itashuka dimbani Jumatatu ya wiki ijayo kupambana na wanankurukumbi Kagera Sugar katika dimba la Kaitaba Mjini Bukoba.

Simba itakutana na Kagera Sugar katika dimba hilo, huku Kagera Sugar ikitoka kupoteza mchezo wao dhidi ya Njombe Mji ya mkoani Njombe katika uwanja wa Sabasaba.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: