Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Arusha Joseph Bukombe ametoa siku 10 kwa wamiliki wa shule binafsi za mchepuo wa kingereza kupeleka magari yanayosafirisha watoto shuleni kwa ajili ya ukaguzi
Akizungumza na wamiliki wa shule hizo na walimu wakuu, mkuu huyo katika kikao kilichowakutanisha wamiliki pamoja na uongozi wa kikosi cha Usalama barabarani mkoani hapo amesema lengo ni kuzungumzia hali ya usafirishaji wa watoto katika shule hizo.
Bukombe amesema sheria ya Usalama barabarani namba 36 kifungu 1(b)kinaeleza namna ya watoto chini ya umri wa miaka mitatu wanavyotakiwa kusafirishwa ambapo wanakuwa chini ya uangalizi wa mzazi au mlezi huku miaka mitatu hadi kumi na mbili akitambulika kama msafiri na anapaswa kukaa kwenye kiti kama ilivyo kwa watu wazima.
Amesema ameona ni vyema kuwaita wamiliki ili kuwaeleza namna ambavyo wamekuwa wakiwasafirisha watoto kama mizigo kwa kuwarundika kwenye magari kinyume na utaratatibu
Kwa upande wa mwenyekiti Msaidizi wa chama cha wamiliki wa shule binafsi maarufu kama Tamongsco Safia Okash ameshukuru kwa utashi uliofanywa na Kikosi hicho cha Usalama barabarani kuwakutanisha ili kuwaelekeza na kuwakumbusha wajibu wao.
Hata hivyo wakiongea kwenye kikao hicho baadhi ya wamiliki hao wameomba kupatiwa muda wa kurekebisha magari mabovu ambapo wameshauri busara itumike katika kutoa adhabu kwa watakao bainika na makosa kulinangana na uwezo wa shule husika.
Post A Comment: