Serikali imewafukuza kazi waalimu 28 baada ya kubainikia walikuwa wakichukua mshahara muda mrefu bila kufanya kazi visiwani Zanzibar mbali na kufukuzwa kazi, walimu hao wanatakiwa kurudisha fedha hizo ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 100.
Akizungumza na waandishi wa habari Ikulu Mjini Zanzibar leo Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya mapinduzi Zanzibar, Abdul-Hamid Yahya Mzee, amesema, pamoja na kufukuzwa kazi waalimu hao waliokua wakichukua mishahara hewa lakini pia wanatakiwa kulipa fedha hizo serikalini.
Amesema uamuzi huo umekuja baada ya uhakiki kufanyika katika Wizara mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na kubaini kasoro ambazo watendaji wake walionekana kufanya makosa hayo kwa makusudi.
Amesema sababu za kufukuzwa kwa walimu hao ni kuchukua fedha za mishahara bila ya kuwepo kazini kwa muda mrefu huku wakishindwa kabisa kutoa taarifa kwa wahusika.
 
Share To:

msumbanews

Post A Comment: