Mshambuliaji wa Manchester United, Alexis Sanchez pamoja na klabu yake ya awali ya Arsenal, wameingia matatani baada ya kukosa kipimo cha dawa za kulevya.
Taarifa iliyotolewa na Chama cha Soka England (FA) inaeleza kwamba Sanchez hakwenda kufanya kipimo cha dawa za kulevya siku ambayo alikamilisha uhamisho wake kwenda Manchester United Jumatatu wiki hii.
Mchezaji huyo alikamatwa Uingereza na taasisi ya kuzuia dawa za kulevya ambapo ilieleza kuwa Arsenal ndiyo hawakuwapa taarifa FA kwamba mchezaji huyo asingejumuika nao kwenye mazoezi.
Raia huyo wa Chile huenda akakabiliwa na adhabu baada ya kukosa kipimo hicho siku aliyojiunga na Manchester United.
Maofisa wa FA walikuwa wakimsubiri mshambuliaji huyo huku lakini Sanchez  hakutokea kufanyiwa vipimo.
Hata hivyo, Arsenal ndiyo waliotakiwa kuwapa taarifa FA kutokana na mabadiliko yoyote ya ratiba ya mazoezi kila siku siku ambayo Sanchez hakuhudhuria mazoezi yao.
Hata hivyo, Arsenal hawawezi kujiweka mbali na adhabu inayoweza kutolewa kutokana na kuhusika kukwamisha vipimo vya dawa za kulevya kwa mchezaji huyo.
Licha ya Arsenal kumruhusu Sanchez kujiunga na United, hata hivyo wanaweza kukumbwa na adhabu iwapo FA haitaridhika na maelezo yao.
Hata hivyo, kosa hilo halimzuii Sanchez kucheza leo Ijumaa kwenye mechi ya Kombe la FA dhidi ya Yeovil Town.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: