Kampuni ya madini ya Acacia imesema kuwa uzalishaji katika robo ya nne ya mwaka 2017 umepungua kutokana na kuzuiwa kusafirisha makinikia ya dhahabu na shaba kwenda nje ya nchi.
Katika taarifa yake iliyotolewa imeeleza kwamba uzalishaji wake katika miezi mitatu ya mwisho hadi Disemba 2017 imepungua kwa asilimia 30 hadi tani 4.2 kuliganisha na kipindi kama hicho mwaka uliopita, lakini pia uzalishaji umepungua kwa asilimia 22 ukilinganisha na robo ya tatu ya mwaka 2017.
Kampuni hiyo ilipunguza kwa kiasi kikubwa uzalishaji katika mgodi wa Bulyanhulu kuanzia Septemba mwaka jana kufuatia mgodi huo kuzalisha hasara baada ya serikali kuzuia usafirishaji wa makinikia tangu mwezi Machi.
Serikali ya Tanzania ilizuia usafirisha huo ikiamini kwamba haipati mapato stahiki na hivyo ikahimiza ujengwaji wa kinu cha kuchenjulia makinikia hapa nchini.
Kiongozi wa mpito wa Acacia, Peter Geleta amesema bado wanaendelea na mchakato wa kufikia makubaliano na serikali ya Tanzania kuhusu namna nzuri ya kufanya biashara.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: