Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amewapa onyo wanasiasa wilayani hapa akisema atawachukulia hatua kali pindi watakapochochea migogoro ya ardhi kwa wananchi wake.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Njoro, Mnyeti alisema yeye siyo Mkuu wa Mkoa wa maboksi ambaye anaogopa kunyeeshewa na mvua hivyo mwanasiasa yeyote ambaye atachochea migogoro ya ardhi ndani ya mkoa wake ajue hatobaki salama.

" Tumekuwa na migogoro isiyokwisha wewe una shamba lako kule kijiji cha bwawani kuna mtu anakuzuia kulima hapa njoro? au ukiishi hapa Njoro kuna mtu anakunyima kununua nyumba kule Kibaya makao makuu ya wilaya? alihoji Mnyeti.

Alisema wanasiasa wengi wamekuwa wakichukulia migogoro ya ardhi kama mtaji wa kujinufaisha wenyewe kisiasa na kwamba hatowavumilia wale wote wanaochochea migogoro hiyo baina ya mtu na mtu au kijiji kwa kijiji.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: