Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti ameivunja Serikali ya Kijiji cha Emboreet wilayani Simanjiro, kwa kukwamisha shughuli za maendeleo kwa sababu ya madai ya Sh30 milioni ya posho ya vikao.

Mnyeti amefikia uamuzi huo baada ya wajumbe 14 wa serikali ya kijiji hicho kudai Sh30 milioni za posho ya vikao jambo alilosema halipo kisheria.

Amesema wajumbe hao waliamua kila mmoja alipwe Sh30,000 za posho ya kikao, huku mwenyekiti wa kijiji hicho, John Olendikoni akilipwa Sh40,000.

Mnyeti amesema Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Yefred Myenzi hakuidhinisha malipo hayo hivyo kuwa chanzo cha kukwamisha maendeleo.

Mwenyekiti wa kijiji hicho ambaye pia  alituhumiwa kufuja Sh4 milioni alizirudisha na baadaye alijiuzulu nafasi hiyo mbele ya mkuu wa mkoa.

Mnyeti amemwagiza Myenzi kuitisha uchaguzi mpya kujaza nafasi hizo baada ya siku 30 kuanzia jana Jumanne Januari 23.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: