Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mhe. Paul Makonda Jumamosi hii ameshindwa kujizuia na kutoa machozi ya uchungu baada ya kumsikiliza mama mstaafu ambaye amedai kudhulumiwa nyumba yake Plot 61, Block B iliyopo Tegeta Jijini Dar es Salaam na mfanyabishara mmoja ambaye walimuazima pesa kwaajili ya kulipia mkopo benki.
Mama huyo amedai alimkopa mfanyabishara huyo tsh milioni 20 kwa makubaliano ya kuzirejesha kwa riba lakini mfanyabiashara huyo alienda kutengezea mkataba feki ambao unaonyesha nyumba hiyo ameinunua kwa tsh milioni 96.
Alisema hata alivyojaribu kumtafuta mfanyabishara huyo ili wamrejeshee pesa zake aliwapiga chenga na alivyompata alikataa milioni 20 na kudai alipwe milioni 300 ili wajereshewe nyumba yao. Kwa sasa wastaafu wao wamesaidiwa nyumba ya kuishi baada ya kufukuzwa kwenye nyumba yao.
Post A Comment: