Paul Christian  Makonda, Rc wa Dar es salaam nadhani nje ya Chuki na Maneno na mihemko utakubaliana na mimi Makonda kawazidi mbali sana  Kwa akili hawa Wengine

Kumekuwa na chuki tu na husda za kijinga sana, Mimi hata vyombo vya habari vilivyomfungia mimi nilikataa sababu Makonda ukimtazama bila hisia za Ubinafsi anaweza kuwa tafsir sahihi ya Mtumishi wa Umma (servant leader)

 lazima tukubali kuwa huyu ndiye Rc Bora aliefanikiwa kucheza mziki wa Dr Pombe, Wengine naona Wamelewa Pombe kali ya Dr Pombe

Hatuwezi kuwa na Ma RC kazi kutoa zawadi za Biko, Ma Rc kukimbizana na Waendesha Boda boda huku Hospital za wilaya hazina Hata Miundo mbinu mpaka serikali kuu ilete wakati kuna watu wameaminiwa ,yaani Wapo tayari kuona Mtu anafia mlangoni mwao kisa Serikali kuu haijaleta hela, Makonda kafanikiwa kuleta Meli na kuanza kutibu watu, hata kama alisaidiwa na Chuma kuwaleta wachina kwani wengine Chuma kimewazuia, Hapa ndipo akili za Makonda unaweza kuzitofautosha na Hawa wa Kugongewa hodi na Biko kutoa zawadi, huku Mwanza Pamba inakufa, Kagera Hakuna tena Ndizi wala kiwanda cha kutisha


Rc Makonda Hatupi lawama kwa mtu, Barabara
Hata ziwe chini ya Jiji zikiwa mbovu anapita nao, ila kwetu huku Ma Rc utawasikia hiyo iko jiji nendeni kwa mkurugenzi

Ma Rc wetu huku ni kuzindua tu kikundi cha waendesha Boda Boda badala hiyo kazi ifanye na polisi kitengo cha usalama barabarani

Watu wa Dar Mnamaneno mengi sana kumsimanga Rc Makonda lakini ukweli Mmebahatika, Vita ya Dawa za kulevya alipoanzisha nikao Ma Rc wengine wakadakia ameacha na wenyewe moto umekata

Rais Magufuli Amesikika mara mbili akisema I wish wakuu wa mikoa mingine wafanye kama Makando (hii ilikuwa meseji kuwa hamfanyi lolote)

Rc wangu wa Mwanza mimi bado sijamuelewa, Nimekuwa namuona kwenye  kwenye

1.Kuchoma Nyavu za wavuvi

2.Gari lilipo tumbukia kwenye Maji

3.Kukagua kama Machinga wamefukuzwa mjini

4.Majambazi wamevamia sehemu,
Hii ni aibu, mimi kama mwandishi naona udhaifu mkubwa, Rais magufuli, Rais Magufuli, Rais Magufuli washa jicho lako kwenye Mikoa, washa Moto, naomba uwakwe uwakwe hasira kwa dakik Kumi, ili mtikisiko upite Labda wataelewa

Haya Kule Moshi, Arusha wanaonekana kwenye Vita ya ubabe tu usio na tija, Wengine kushambulia shamba la Mbowe na Mwingine kupokea madiwani

Bora huyu anaetuhumiwa na kusimangwa kuwa Bashite na Tuhuma za kwamba hajasoma  na amenunua majina lakini kuna kwenye majina yao lakini ni hovyo tupu

Note Katika Ma Rc wanaofanya mambo hovyo Mtaka si miongoni Mwao alianza vizuri ila kuna speed imepungua, yule ni Kaka yangu nitamuuliza imekuwaje

Kama hauna haya popote taja Rc mbovu na ili kwenye kusafisha tunsaidie Rais

Usiogope katiba inasema Mamlaka ya hawa viongozi  msingi wake ni sisi wananchi hivyo tunauwezo wa kusena kama wanatuharibia nchi

Alloyce Nyanda
Mtozi
Share To:

msumbanews

Post A Comment: