Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda leo amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa Mabasi 11 ya Vyombo vya ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Police, Magereza na Jeshi la wananchi ambapo hadi Mwishoni mwa mwezi huu baadhi yatakuwa yamekamilika na kukabidhiwa.

Magari hayo ni yale yaliyopelekwa Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani yakiwa chakavu (Screpa) na sasa yapo katika hatua ya mwisho kukamilika yakifungwa vifaa vya kisasa ikiwemo AC, chaji ya simu, TV, viti,  bodi mpya, taa, side mirrors, tairi, vioo huku baadhi zikiwekewa vyoo vya ndani.

RC Makonda ameeleza kuridhika na kasi ya ujenzi huo ambapo ameshukuru kiwanda cha Dar Coach Ltd kwa uzalendo wa kujitolea kukarabati magari hayo.

Aidha RC Makonda amesema maboresho ya magari hayo 11 yameisaidia Serikali kuokoa kiasi cha zaidi ya shillingi illion moja ambazo serikali ingetumia lakini kampuni hiyo imejitolea kukarabati magari hayo bure.

Nao Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama walioambatana na RC Makonda akiwemo Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dsm Lazaro Mambosasa, Mkuu wa Jeshi la Magereza DCP Agustin Mboje na Kaimu Mkuu mkuu wa Usafirishaji JWTZ Canal Benjamin Kisinda wamempongeza RC Makonda kwa ubunifu anaoufanya ambapo wamesema Magari hayo yatasaidia kuimarisha ulinzi na usalama pamoja na kuwafanya Askari kufanya kazi katika mazingira mazuri.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kiwanda cha Dar Coach Ltd Bwana Manmeet Lal amemuhakikishia RC Makonda kuwa magari Matano Kati ya 11 yatakabidhiwa mwishoni mwa mwezi huu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: