Polisi mkoani Katavi wamefanikiwa kuwaua watu wawili wasiofahamika wanaodhaniwa kuwa ni majambazi katika majibizano ya risasi.
Alisema kabla ya tukio hilo, polisi walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kijijini hapo kuna watu ambao ni wageni na hawaeleweki mienendo yao, ambapo walihofia huenda wakawa wamefika kufanya ujambazi. Alisema baada ya taarifa hizo polisi walianza kufanya msako wa kuwatafuta watu hao, ambao wapo watano kisha walianza kuandaa mtego wa kuwakamata.
Alisema kabla ya kuwakamata walishtukia mtego huo na kuanza kuwarushia polisi risasi ambapo polisi nao walijibu mapigo na kuwaua wawili na kuwakamata watatu na waliwakuta wakiwa na bunduki tatu aina ya SMG na risasi 16 pamoja na magazini tano. Kamanda Nyanda alisema watu hao walikutwa na vipande vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 6.6 yakiwa na thamani ya zaidi ya Sh. milioni 34 pamoja na nyama ya pofu kilo 20 yenye thamani ya Sh. milioni nne.
Post A Comment: