POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imesema wamepokea shauri la Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Augustine Mrema la kutaka aliyemzushia kifo akamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kamanda wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa alisema jana kuwa walipokea shauri hilo la Mrema ambae amelitaka Jeshi la Polisi kuchukua hatua kwa mtu aliyeanza kusambaza taarifa hiyo.
“Tunalifanyia kazi suala hilo na jalada litakapokamilika tutalipeleka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa hatua zaidi za kisheria… kuna watu wamekuwa wakiitumia vibaya mitandao,” alisema Kamanda Mambosasa.
Hivi karibuni mitandao balimbali ya kijamii ilisambaza taariza za uzushi za kifo cha Mwanasiasa huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Parole, lakini baadae alikanusha taarifa hizo na kusema kwamba ni mzima wa afya.
Wakati huo huo, alisema mtuhumiwa anayedaiwa kumuua mtoto, mkewe na shemeji yake kwa jembe amekamatwa mkoani Iringa na wanafanya utaratibu wa kumrejesha Dar es Salaam kwa ajili ya hatua za kisheria.
Katika tukio lingine, Kamanda Mambosasa alisema kwamba wanafuatilia taarifa za mwanamke anayedai kutapeliwa nyumba na viwanja vyake na itakapokamilika pia watatoa taarifa.

“Nimepokea taarifa za mwanamke huyo kutapeliwa ila hiyo ilionekana kwenye vyombo vya habari inafanyiwa kazi na polisi Makao Makuu, isipokuwa leo sisi tumepokea taarifa nyingine ya hati ya kughushiwa na tunazifanyia kazi na hatujui kama mtuhumiwa ni mchungaji au la ila itakapokamilika tutawajulisha” alisema Mambosasa
Share To:

msumbanews

Post A Comment: