Hii ni nyumba aliyokuwa akiishi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1959 mara baada ya kujiuzulu kazi yake ya ualimu katika Shule ya Sekondari ya Mt. Francis Pugu (sasa Shule ya Sekondari Pugu) Machi 22, 1955.
Mwalimu Nyerere alijiuzulu kazi yake ili apate muda wa kutosha kuendeleza harakati za kisiasa za kupigania uhuru wa Tanganyika chini ya TANU.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalla amesema kuwa, nyumba hii iliyopo eneo la Magomeni jijini Dar es Salaam itafanyiwa marekebisho na kutangazwa kwani ni kivutio kikubwa cha utalii.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: