Jeshi la Polisi nchini Tanzania limewakamata ‘majambazi’ kadhaa walipokuwa katika jaribio la kutaka kufanya uhalifu kwa wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Babati mkoani Manyara leo Januari 24, 2018.
Tukio hilo lilikuwa ni la kutengeneza ambapo polisi walikuwa wakifanya mazoezi kwa ajili ya kujiimarisha.
Mara kwa mara Jeshi la Polisi Tanzania hufanya mazoezi katika mazingira halisi ambapo tukio linaweza kutokea, kwa ajili ya kujiweka tayari kukabiliana au kuwalinda raia pamoja na mali zao.
Post A Comment: