Kiongozi wa Muungano wa Upinzani nchini Kenya (NASA), Raila Odinga, jana Jumanne, Januari 30, aliapishwa kuwa ‘rais wa wananchi’ nchini humo, baada ya kusema hatambui ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa marudio uliofanyika Oktoba mwaka jana.
Mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka wa chama cha Wiper hakujitokeza katika sherehe hiyo ya kuapishwa, ingawa alikuwa miongoni mwa watu waliotarajiwa kuapishwa.
Raila Odinga alitangaza kuwa Kalonzo Musyoka ataapishwa baadaye.
Hili siyo tukio la kwanza la baadhi ya watu kutangaza kujiapisha kama marais w nchi zao barani Afrika na ulimwenguni kwa ujumla. Wapo viongozi wengi, hasa wa vyama vya upinzania ambao wamekuwa wakitangaza kujiapisha, kutokana na kutokubaliana na ushindi wa kiongozi aliyeo madarakani.
Mfano viongozi wa nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo – Etienne Tshisekedi, Nigeria – Moshod Abiola, Uganda – Kiza Besigye na Jean Ping wa Gabon ni miongoni mwa viongozi wa upinzani wa Afrika ambao wamejaribu kujitangaza kuwa marais.
Etienne Tshisekedi
Etienne Tshisekedi alikuwa kiongozi mkuu wa upinzani, wakati wa utawala wa Rais Mobutu Sese Seko Zaire, na baadaye Laurent Kabila Joseph Kabila wa DRC
Kufanana kati ya Tshisekedi na Odinga ni kwamba wote wawili walikuwa kizuizini bila kufunguliwa mashtaka, wote walihudumu kama mawaziri wakuu na wote waligomea uchaguzi wa urais; Tshisekedi mwaka 2006, Odinga katika 2017.
Mwezi Novemba 2011, Tshisekedi alijitosa kwenye kinyang’anyiro dhidi ya mtoto wa Laurent Kabila, kisha aliamua kujiandalia kiapo mwenyewe na kuapishwa nyumbani kwake na mkuu wa watumishi wake Albert Moleka baada ya jaribio la kujiapisha katika uwanja wa Wahanga, Kinshasa kutibuka. Baadaye, aliwekwa katika kizuizi cha nyumbani.
Moshood Abiola
Nigeria, Moshood Abiola alijitangaza mwenyewe kuwa rais kipindi ambacho Rais Sani Abacha alipokuwa madarakani.
Hii ni baada ya kutembelea nchi nyingi za Magharibi, kutafuta msaada ili kumkabili Abacha katika utawala wake.
Alikamatwa na kushtakiwa kwa uhaini na kufungwa jela kwa miaka minne hadi ilipofika mwaka 1995, Siku aliyoachiwa kutoka gerezani, alikutana na ujumbe wa Marekani na kuhuduria mkutano.
Baada ya kupewa chai akiwa mkutanoni alianguka na kuzimia na hatimaye kufariki dunia.
Jean Ping
Mwaka 2016 Gabon, kiongozi wa upinzani Jean Ping alijitangaza mwenyewe kuwa rais na kutoa wito kura kurudiwa kuhesabiwa kwa kura ambazo zilithibitisha kwamba Ali Bongo ameshinda.
Hata hivyo dunia nzima alijua kwamba Ping ndiye alikuwa rais wa nchi hiyo
Kizza Besigye
Nchini Uganda Kiongozi wa upinzani Kizza Besigye, ambaye ni mpinzani wa muda mrefu wa Rais Yoweri Museveni, kupitia kanda ya video alionekana akifanya sherehe za kula kiapo kuwa Rais wa Uganda baada yake kushindwa uchaguzini mwaka 2016 na Bw Museveni.
Alikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uhaini.
Source – BBC
Share To:

msumbanews

Post A Comment: