Mwache Okwi aringe tu! Ndiyo unachoweza kusema baada ya mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi kufunga mabao mengi kuliko timu saba (7) za Ligi Kuu Bara hadi sasa.
Okwi kwa sasa anaongoza katika orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu Bara akiwa na mabao 12 na kuisaidia Simba kuongoza ligi kwa pointi 35.
Idadi ya mabao aliyofunga Mganda huyo katika ligi hadi sasa ni mengi kuliko yaliyofungwa na klabu saba (7) katika michezo 15.
Timu zinazozidiwa kwa mabao na Okwi ni pamoja na Mtibwa Sugar iliyofunga mabao 11, nyingine ni Ndanda (9),  Ruvu Shooting (9), Lipuli (8), Njombe Mji (8),Kagera Sugar (7), na Stand United iliyofunga mabao matano tu hadi mzunguko wa kwanza unamalizika.
Mbali ya kuzizidi timu hizo saba kwa kufunga mabao pia Mganda huyo amefunga goli sawa na timu mbili ambazo ni Mbeya City na Majimaji zilizofunga mabao 12 kila moja.
Okwi pamoja na kuwa hajafunga bao lolote nje ya Dar es Salaam hadi sasa bado amewaacha wenzake katika orodha ya wafungaji kwa mabao matano.
Washambuliaji waliofunga mabao saba (7) hadi sasa ni Habib Kyombo wa Mbao FC, Mohammed Rashid (Prisons), Obrey Chirwa (Yanga), John Bocco      (Simba).
Winga wa Simba, Shiza Kichuya amefunga mabao sita (6) wakifuatiwa na  Ibrahim Ajib wa Yanga mabao 5, sawa na Asante Kwesi      (Simba), na Marcel Boniventure wa Majimaji.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: