Nyumba yenye vyumba 15 vya  wapangaji wa kuishi na maduka inayomilikiwa na mfanyabiashara Hussein Gonga iliyopo eneo la Kaloleni jijini Arusha imeungua kwa moto uliozuka jana majira ya saa 9 alasiri na kuteketeza kila kitu na kusababisha  familia 11 kukosa mahala pa kuishi.

Tukio hilo lilitokea majira ya SAA 9 alasiri huku chanzo cha moto huo kikielezwa kuwa ni hitilafu ya umeme.

Kwa mujibu wa Diwani wa kata ya kaloleni ,Emanuel Kessy amesema kuwa alipata taarifa za tukio hilo na kufika eneo la tukio,ambapo alikuta moto mkubwa ukiwaka kwa nguvu huku jeshi la zima moto ambao walichelewa kufika walishindwa kuudhibiti mapema kutokana na Magari yao kuishiwa Maji mara kwa mara  jambo lililopelekea kuunguza kila kitu na vitu vichache viliokolewa.

Kwa mujibu wa waathirika wa tukio hilo ,moto huo umechukua takribani masaa Masaa manne kuanzia SAA 9 alasiri hadi majira ya SAA 12 jioni ndipo kikosi cha zima moto walipofanikiwa kuuzima.

Katika tukio hilo.hakuna taarifa za  aliyejeruhiwa kutokana na wapangaji wengi kuwa makazini na polisi waliimarisha ulinzi ili kudhibiti matukio ya uporaji.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: