Azam na Yanga zitapamabana kesho saa 10:00 jioni kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Afisa Habari wa Yanga, Dismas Ten amesema timu hiyo itawakosa Amissi Tambwe,Thaban Kamusoko, Yohana Mkomola, Donald Ngoma, Pato Ngonyani, Abdallah Shaibu 'Ninja' walio majeruhi pamoja na Pius Buswita mwenye kadi tatu za njano.

Timu hiyo ilifanya mazoezi ya mwisho jana huku Tambwe akifanya kidogo na kupumzika wakati wengine hawakushiriki kabisa.

Ten alisema wanaiheshimu Azam kwani wamekuwa na msimu mzuri lakini  hata Yanga ipo vizuri na ipo tayari kuvuna pointi tatu katika mchezo huo.
"Azam ni timu nzuri na imekuwa ikipata matokeo katika uwanja wao na hata ugenini ila ata sisi Yanga tupo vizuri na tunatarajia kupata matokeo kwenye mchezo wa kesho."alisema Ten.

Kuhusu  suala la kocha George Lwandamina ambaye hakukaa benchi michezo miwili kutokana na kutokuwa na kibali cha kazi,Ten alisema taratibu zote za kibali cha kocha huyo zimefuatwa na kufanyiwa kazi hivyo mashabiki na wanachama wa klabu hiyo wasiwe na hofu.



Share To:

msumbanews

Post A Comment: