MSANII chipukizi wa Bongo Fleav, Nini amefunguka kuhusu uhusiano wake na Nay wa Mitego na kueleza kuwa hajawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na rapper huyo.
Kauli ya Nini anakuja baada ya hapo awali kuwepo taarifa kuwa sababu ya kutimuliwa MJ Record ni kuwa na mahusiano na Nay.
“Sina mahusiano ya kimapenzi na Nay, halafu hata kama ningekuwa nayo, kiupande wangu I don’t real think hiyo ni sababu ambayo ingeweza kumfanya yeye afanye kile alichokifanya,” amesema.
“Seriously sidhani kama mahusiano ya kimapenzi yanaweza kuathiri muziki, sina uhakika may be according to me navyofikiria lakini sidhani kama hiyo it can be specific reason,” amesisitiza
Post A Comment: