Msanii Nay wa Mitego amelalamikia kitendo cha watu wasiofahamika kudukua acount zake za instagram na Youtube, na kufuta vitu vyake vyote
Akizungumza na mwandishi wa Eatv Nay amesema watu hao walianza na acount yake ya instagram na kisha kuingia Youtube, na kufuta kazi zake zote alizofanya tangu anaanza muziki.
"Yaani wamehack acount yangu ya instagram, ilikuwa na followers zaidi ya milioni moja, usiku wakaingia kwenye YouTube wakafuta kazi zangu zote, yani mtu anafuta vitu bila huruma, sijui kwa nini tunachukiana hivi, wasanii wenyewe tupo wachache lakini tunachukiana hivi", amesema Nay wa Mitego.
Kufuatia tukio hilo Nay wa Mitego amesema tayari amezungumza na mtaalamu wa masuala  ya mtandano Mx Carter, ili kumrudishia acount zake
Share To:

msumbanews

Post A Comment: