Nasikia Mwanamke mmoja anaitwa Joyce Kiria kashambuliwa na Mtu mmoja (mmewe) kwa kupigwa na Kugongezwa kichwa kwenye Gari anaonekana kulalamika mitaani kitu ambacho ni haki yake! Japo afahamu IGP Siro alisema polisi haifanyii kazi za mitaani aendee polisi
Sasa mimi nina mambo mawili ya kusema japo ninemsikia kiria akilia tu so hii inaweza kuwa ni (the danger of writing a Single story) ila sitahukumu kuwa kileo kakosea (mazingira tu ya nini naona)
1.Nchi yangu haiko serious eeeh, inaonekana Bado hakuna dhamira ya kuheshimu na kulinda wanawake, jitu linamvamia mkewe, linamtwanga, linadunda mitaani, Serikali ipo, waziri mpo, Mwanamke mpaka anajitokeza kulalamika nje ujue hana imani na Serikali yake, Ameshindwa hata kwenda polisi, nchi za watu kama Dernamak huyu kileo angekuwa ameshahukumiwa kufungwa huwezi kucheza na mwanamke kipumbavu namna hii nchi ikacheka cheka, jamii ikacheka cheka kipumbavu, Chama alichopo kingepaswa kumchukulia hatu haraka kiongozi wake mwenye mkono (Bawacha wangemlinda kiria kwa kuomba maandamo ya amani)
Sasa Natoa wito kwa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) mama yangu Dkt Helen Bisimba jitokeze na team yako, vaeni kininja na mimi nitavaa tukakemee vikali na kutia shinikizo Kileo akamatwe haraka na kufikishwa mahakaman kesho na tushinikize afungwe haraka ili sisi wanaume tuwaogope wanawake
2.Na wewe Joyce Kiria usidhani kulipa Kodi ya nyumba ndio Bima tosha kabisa ya kufanya uhalifu (huwezi tu kusema umepigwa tu yaani umekaa akaanza kukupiga kuna jambo umefanya) kama ilitokea tu kakushambulia bila kosa tu basi kileo atakuwa mwehu
Alloyce Nyanda
Mtozi
Post A Comment: