Onesmo Machibya almaarufu Nabii Tito aliyetengeneza vichwa vya habari kutokana na mahubiri yake ya kuhimiza ulevi na uasherati, amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, na kusomewa mashtaka ya kujaribu kujiua.

Nabii Tito alifanya jaribio la kujiua Januari 25, mwaka huu akiwa mahabusu, ambapo inadaiwa kwamba alijikatakata na wembe kwa lengo la kuyakatisha maisha yake.

Alipotakiwa kujibu mashtaka yanayomkabili, Nabii Tito awali alisema hakumbuki chochote kwa sababu yeye ni mgonjwa wa akili, lakini alipobanwa kwa mara nyingine, alisema ni kweli alitaka kujiua kwa sababu kuna sauti ndani ya kichwa chake iliyokuwa inamuelekeza kufanya kitendo hicho.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Nabii Tito amerejeshwa rumande huku akiwekewa mapingamizi saba ya dhamana.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: