Aliyekuwa mbunge wa Kinondoni (CUF), kisha kuhamia CCM, Maulid Mtulia leo Januari 17, 2018 amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea wa jimbo hilo kwa tiketi ya chama tawala.

Amechukua fomu hizo hizo za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika ofisi za manispaa ya Kinondoni.

Hatua hiyo imekuja baada ya siku nane zilizopita Mtulia kutii agizo la chama hicho lililomtaka kuripoti ofisi ya CCM mkoa kwa ajili ya kuchukua maelekezo ya uchaguzi.

Hivi karibuni CCM kilitangaza kuwarudisha kugombea majimbo yao waliokuwa wabunge, Mtulia wa Kinondoni na Dk Godwin Mollel (Siha-Chadema) ambao wamejiunga na chama hicho tawala.

Mtulia alipoulizwa nini ambacho anawaeleza wananchi wa Kinondoni, amesema siku ikifika atazungumza mengi.

Uchaguzi mdogo wa marudio wa majimbo ya Kinondoni na Siha unatarajiwa kufanyika Februari 17 baada ya NEC, kupokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge Job Ndugai ikieleza majimbo hayo yapo wazi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: