Mtoto mwenye umri wa miaka kumi na moja amekutwa akiwa amejinyonga katika eneo la Ongata Rongai Nchini Kenya katika mazingira ya kutatanisha.
Mtoto huyo wa kiume ambaye alikuwa akiishi na mama yake pamoja na mdogo wake wa kike alikutwa juzi jioni akiwa ananing’inia kwenye kamba.
Tukio hilo lilibainika baada ya mdogo wake huyo mwenye umri wa miaka sita kurejea nyumbani na kukuta mlango ukiwa umefungwa kwa ndani na jitihada zake za kujaribu kufungua na kuita hazikufanikiwa kwani hapakuwa na mtu aliyeitikia.
Kutokana na kugonga mlango na kuita kwa muda mrefu, majirani akiwamo mwenye nyumba walikwenda kumsaidia na walikubaliana kwamba waondoe chuma kilichokuwa katika mlango ili kumwezesha binti kuingia ndani na kumkuta kaka yake akiwa ananing’inia kwenye kamba.
Majirani hao walitoa taarifa katika kituo cha Polisi Rongai ambao walifika na kuchukua mwili wa marehemu na kuuhifadhi katika chumba cha kuhifadhia maiti cha jiji huku wakiendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: