Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Finland Pekka Hekka juu ya utekelezaji wa mradi wa TANZIS.
Mazungumzo hayo yamefanyika mkoani Dodoma katika ofisi za Waziri.
Lengo la mradi wa TANZIS ni kukuza ujuzi na ubunifu kwa lengo la kuongeza mianya ya ajira, na kuwa mradi huo unatarajiwa kuanza mapema mwaka huu na utafadhiliwa na Serikali ya Finland.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Dkt Amos Nungu ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu.
Imeandaliwa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA.
16/1/2018
Post A Comment: