Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ameongeza mkataba wake wa kukaaOld Trafford, hadi 2020.
Mreno huyo ndiyo kwanza yuko mkataba wake wa awali wa miaka mitatu ulitarajiwa kufikia mwisho mwakani.
Lakini Man United imetangaza kuwa Mourinho ambaye kesho Ijumaa atatimiza miaka 55, amekubali kuongeza mwaka mmoja wa mktaba wake wa sasa.
Mourinho ametwaa mataji matatu katika msimu wake wa kwanza Old Trafford, alisema: 'Nimefurahi kupata heshima hii ya kuwa kocha wa Manchester United.
"Ningependa kusema asante kwa wa mmiliki na Woodward kwa kutambua mchango wangu na kujitoa kwangu hapa. Nimeona jinsi uaminifu wao ulivyokuwa mkubwa juu yangu ya kuendelea kuwa kocha hapa.
"Tumeweka viwango vikubwa kwa kutwaa mataji matatu katika msimu wa kwanza, lakini hivyo ndivyo vya viwango vya timu zangu. Tumetegeneza mazingira mazuri ya kuifanya Manchester United kuwa klabu bora zaidi kwa siku za baadaye."
Share To:

msumbanews

Post A Comment: