Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa atakuwa na kibarua kizito mbele ya mabeki wa Azam, Yakubu Mohammed na Aggrey Morris wakati mchezo wa timu hizo leo saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Chirwa kinara wa ufungaji wa Yanga akiwa na mabao saba (7), anarejea uwanjani baada ya kumaliza adhabu ya kufungiwa michezo mitatu akiwa amebeba matumaini yote ya mabingwa hao katika kuhakikisha wanashinda.
Mzambia huyo anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa safu ya ulinzi ya Azam inayoongozwa na kipa Razack Abalora na mabeki, Mohammed na Morris ambao wametengeneza ukuta wa chuma ulioruhusu mabao manne tu katika michezo 14 walizocheza hadi sasa.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: