KUFUATIA video ya mama mjane iliyosambaa mitandao ikimuonyesha akilalamikia baada ya nyumba yake kupigwa mnada, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliagiza mama huyo atafutwe na afike ofisini kwake leo saa tatu asubuhi jambo ambalo mama huyo ameliekeleza.

Mjane huyo, Bernadetha Ryewendera mkazi wa Teget,a Mtaa wa Upendo ambaye anadai nyumba yake ilipigwa mnada January 12 mwaka huu kwa dakika tano bila yeye kupewa taarifa yoyote, amefika ofisini kwa Makonda leo ambapo baada ya kupitia nyaraka zake, RC Makonda ameagiza kusimamisha mnada wa nyumba hiyo aliouita ni batili.

Akizungumza na waandishi wa habari Makonda amesema kuwa katika uchunguzi wa awali uliofanywa na wanasheria umeonesha kuna utapeli mkubwa uliofanywa ambao umegushi sahihi ya Bi Zainabu Kaswaka ambaye ni mmiliki wa eneo alilouziwa Bi Rweyendera.

Pia amesema kuwa mnada huo haukuwa halali kwni ulikiuka sheria kutokana na nyumbani iliyopigwa mnada ilikuwa na zuio mahakamani tangu mwaka jan.

Mbali na hilo, Makonda ametoa agizo kuwa mama huyo asibuhgudhiwe na aendelee kuishi kwenye nyumba yake kwa amani.

Aidha Makonda ameagiza watuhumiwa wa utapeli huo kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sharia.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: