Mke wa Tito Machibya Maarufu kwa jina la Nabii Tito, Agnes Miri (36), leo ameweka kambi  Kituo Kikuu cha Polisi mkoani Dodoma, akishinikiza mume wake atolewe kwani amekuwa akiishi maisha magumu.
Nabii huyo ambaye jana alijaribu kujiua kwa kujikata na wembe tumboni na kushonwa nyuzi 25, akiwa chini ya Jeshi la Polisi bado anashikiliwa na jeshi hilo.
Akiwa na watoto wake watatu katika viunga vya polisi, mke wa nabii huyo ambaye amekuwa akionekana na mume wake wakicheza muziki na kunywa pombe, ameiambia Tovuti hii kwamba anaomba jeshi hilo limwachie mume wake kwani maisha yamekuwa magumu kwake.
Amesema yeye na watoto wake wanaumwa ugonjwa wa kuhara na  kutapika ambapo kutokana na mume wake ambaye ndiyo mwangalizi wa familia kushikwa  na polisi  hana mtu wa kumsaidia.
“Maisha yangu ni magumu mimi naliomba Jeshi la Polisi pamoja na Serikali imwachie mume wangu kwani yeye ndiyo kila kitu kwangu ninavyokwambia hapa tangu jana sijatia kitu chochote tumboni na hawa watoto unawaona wanalia tu sababu ya njaa na pia wanaumwa wanatapika na kuharisha.
“Asubuhi jirani alinipa buku (Sh 1,000) ndiyo nimeitumia kama nauli kuja hapa kituoni sasa mimi sitoki hadi wamtoe mume wangu wamtoe yeye ndio kimbilio langu, amesema.
Pamoja na mambo mengine, Agnes amehoji kama Hospitali ya Magonjwa ya akili ya Mirembe wamempima na kugundua Nabii Tito ana matatizo ya akili ni kwanini waendelee kumng’ang’ania.
“Wamesema yule ni kichaa sasa kwanini wanamng’ang’ania wananifanya mimi maisha yangu yawe magumu,” amesema
Share To:

msumbanews

Post A Comment: