Mgombe Ubunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia amewataka wananchi wa jimbo hilo kumchagua kwa sababu sasa hivi amekuwa karibu zaidi na Rais Dkt Magufuli, hivyo ataweza kufikisha matatizo ya wananchi na kupatiwa ufumbuzi mara moja.
Mtulia ameyesema hayo leo katika ufunguzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge ambapo amewaeleza wananchi kwamba, kwa kipindi cha miaka miwili ambacho amekuwa mbunge wa Chama cha Wananchi (CUF) hakuwa na namba ya Rais, lakini sasa anayo, hivyo ataweza kuwasilisha matatizo yao yatatuliwe.
Mtulia amewaambia wanachi wa Kinondoni kwamba amefanya mengi katika jimbo hilo ikiwamo kuzuia bomoa bomoa ya nyumba, hivyo akawasihi wampe nafasi aendelee kuwatumikia.
Aidha, kwa upande wake Salum Mwalimu ambaye ni mgombe ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenye jimbo hilo, ameeleza sera zake na kusema, wananchi wamechague yeye kwa sababu ni mtu ambaye ni ujasiri na atazungumzia, kupigania demokrasi na kusimamia haki.
“Nilitumia kalamu yangu miaka tisa kulitetea jeshi la polisi, nategemea polisi mtalipa fadhila mtaniongezea gia nikawatetee bungeni” alisema Mwalimu.
Uchaguzi mdogo katika jimbo la Kinondoni na Siha unatarajiwa kufanyika Februari 17, 2018.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: