Mgombea Ubunge  wa jimbo la Siha kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Godwin Mollel amefarijika kuona bendera ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenye mkutano wake wa Makiwalu wakati akifanya kampeni za kugombea Ubunge wa jimbo.

Mollel ambaye alikuwa Mbunge wa Jimbo la Siha kupitia CHADEMA na baadae kujiuzulu na kuhamia CCM na sasa kugombea tena kiti hicho kwa tiketi ya CCM.

Katika mkutano wake wananchi walikwenda na kufunga bendera ya CHADEMA pembeni ya bendera ya CCM na yeye kukiri kuwa bado anawapenda watu ambao walipambana naye awali mpaka kupata Ubunge kupitia CHADEMA.


"Niwaambie makamanda bado nina wapenda na kuwaheshimu ndiyo maana nimefarijika kuona bendera hizi mbili (CHADEMA) na (CCM) zipo hapa lakini mmeniwekea kwa namna nzuri kwamba mmeiweka ile juu na mmeonyesha dalili kwamba tutaishusha hii ya chini tuendelee kujenga Siha, mimi leo ni limao nimekuja kuondoa kichefu chefu cha maendeleo na watu wapate maendeleo" alisema Mollel

Mbali na hilo Dkt. Mollel amedai kuwa anakumbuka mchango wa makanda hao ambao waliweza kusimama na yeye na kulinda kura mpaka siku alipotangazwa kuwa Mbunge wa jimbo la Siha kupitia CHADEMA.  
Share To:

msumbanews

Post A Comment: